... | Fetching Islamic Date...
00:00:00
Rifq Online Platform

 

Sikiliza darsa, soma makala za kielimu, uliza maswali ya kidini, na usaidie uendelezaji wa da'wah.

Makala Mpya (Recent Posts)

Soma Zote
Adab Oct 22, 2026

Chakula ni Udongo

Udongo, ni huu ambao ndio tumeumbiwa, na tutarudi humo bila shaka. Udongo huu pamoja na maji mmea hupata maisha. Mmea utachipua, utastawi, utatoa matunda. Na ndio kwa namna hiyo sisi tunapata chakula. Chakula kitaaamu, kizuuri, ambacho tunakula na kustarehe kwa utamu wa ladha yake. Miili yetu inastawi kwa chakula hicho. Hakika hiyo ni neema kubwa sana ambayo ni wachache hugundua baada ya kutafakari...Lakini neema hii kubwa, inapotumiwa kwa ujinga au uzembe, hugeuka kuwa sababu ya maangamizi. Kwa hakika, chakula si tu ladha ya ulimi bali ni amana mbele ya Mola. Na kwa bahati mbaya, leo hii dunia inazongwa na majanga ya afya yanayotokana na ulaji usio sahihi: saratani, kisukari, shinikizo la damu, uzito mkubwa kupita kiasi, na mengineyo mengi. Vyote hivi vinatazamwa kama matokeo ya kula kupita kiasi, kula bila kuchagua, au kula bila nidhamu.Mtume wa Allah (ﷺ) amesema:مَا مَلأَ ابْنُ آدَمَ وِعَاءً شَرًّا مِنْ بَطْنِهِ، حَسْبُ ابْنِ آدَمَ أَكَلَاتٌ يُقِمْنَ صُلْبَهُ، فَإِنْ كَانَ لاَ بُدَّ، فَثُلُثٌ لِطَعَامِهِ، وَثُلُثٌ لِشَرَابِهِ، وَثُلُثٌ لِنَفَسِهِ.(مسند أحمد، رقم الحديث: 17202، صحيح)"Mwanaadamu hajawahi kujaza chombo kibaya kuliko tumbo lake. Inamtosha mwanaadamu matonge machache ya kuistawisha siha yake. Na akilazimika basi theluthi kwa chakula, theluthi kwa kinywaji, na theluthi kwa pumzi." (Abu Ahmad – Swahih)Huu ni msingi wa afya bora na maisha marefu. Lakini leo watu wanakula kupita kiasi, si kwa haja ya mwili, bali kwa tamaa ya roho. Watu wanakula si kwa lengo la kupata nguvu, bali kwa kutafuta ladha. Na ladha hiyo mara nyingi inatoka kwenye vyakula vyenye kemikali, mafuta mengi, sukari nyingi, na uchafu wa viwandani.Mwenyezi Mungu anasema:يَا أَيُّهَا النَّاسُ كُلُوا مِمَّا فِي الْأَرْضِ حَلَالًا طَيِّبًا"Enyi watu! Kuleni katika vilivyomo ardhini vilivyo halali na vizuri..." (Surah Al-Baqarah: 168)Kula kilicho halali pekee hakutoshi. Ni wajibu pia kula kilicho tayyib (kisafi, kisichodhuru, kilicho salama kwa afya). Leo watu wanalimbikiza vyakula vya haraka (fast food), wakisahau kuwa si kila kisicho haramu ni salama.Je, ni nini madhara ya ulaji mbovu?Kimwili, Ulaji mbovu  huweza kuwa chanzo cha Magonjwa ya tumbo, figo, ini, moyo, na mfumo wa mmeng'enyo.Kiroho, Ulaji mbovu usababisha uzembe wa ibada, huzorotesha akili na hupunguza unyenyekevu.Mtume (ﷺ) alitaja mtu anayesafiri kwa ajili ya ibada, lakini alitaja kwa vipi chakula huathiri ibada, sikiliza:ثُمَّ ذَكَرَ الرَّجُلَ يُطِيلُ السَّفَرَ، أَشْعَثَ أَغْبَرَ، يَمُدُّ يَدَيْهِ إِلَى السَّمَاءِ: يَا رَبِّ، يَا رَبِّ، وَمَطْعَمُهُ حَرَامٌ، وَمَشْرَبُهُ حَرَامٌ، وَمَلْبَسُهُ حَرَامٌ،وَغُذِيَ بِالْحَرَامِ، فَأَنَّى يُسْتَجَابُ لِذَلِكَ؟"Kisha alitaja mtu ambaye huenda safari ndefu, mwenye nywele timtim na mchafu, akinyoosha mikono yake mbinguni akisema: Ee Mola wangu, Ee Mola wangu! Lakini chakula chake ni haramu, kinywaji chake ni haramu, mavazi yake ni haramu, na amelelewa kwa haramu, basi ni vipi dua yake itakavyokubaliwa?" (Sahih Muslim)Tutafanyeje basi?Tule kwa kiasi kulingana na haja ya mwili kwaajili ya kujenga afya.Tule vyakula halali tena safi. Epuka vyakula vyenye kemikali na visivyopitia usafi wa kisharia.Tuwe na ratiba ya kula na kunywa tusikiapo njaa na sio hamu tu ya kula.Hitimisho.. Hakika chakula ni baraka na pia ni mtihani. Ndani yake mna neema lakini pia kuna hatari. Tujifunze kula kama taratibu za kiislamu, kwa nidhamu, kwa maarifa, na kwa takwa bila israfu. Tusikimbilie ladha na tukasahau afya. Tusiishi kwa kula tu, bali tule ili tuweze kuishi ili ibada ziendelee. Na mwisho wetu, ni udongo uleule tuliotokana nao, ambao chakula kilitoka humo.Imeandikwa na Abu Rahma Rajab Abdallah
Soma Makala
Manhaj Oct 22, 2026

Undugu wa Kiislamu

إن الحمد لله نحمده ونستعينه ونستغفره ونعوذ بالله من شرور أنفسنا ومن سيئات أعمالنا من يهده الله فلا مضل له ومن يضلل فلا هادي له وأشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له وأشهد أن محمدا عبده ورسوله.﴿يا أيُّها الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ حَقَّ تُقاتِهِ ولا تَمُوتُنَّ إلّا وأنْتُمْ مُسْلِمُونَ﴾.﴿يا أيُّها النّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِن نَفْسٍ واحِدَةٍ وخَلَقَ مِنها زَوْجَها وبَثَّ مِنهُما رِجالًا كَثِيرًا ونِساءً واتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي تَساءَلُونَ بِهِ والأرْحامَ إنَّ اللَّهَ كانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا﴾.﴿يا أيُّها الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا، يُصْلِحْ لَكُمْ أعْمالَكُمْ ويَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ومَن يُطِعِ اللَّهَ ورَسُولَهُ فَقَدْ فازَ فَوْزًا عَظِيمًا﴾. أما بعد:***فإن أحسن الحديث كتاب الله تعالى وأحسن الهدي هدي رسول الله صلى الله عليه وسلم وشر الأمور محدثاتها فإن كل محدثة بدعة وكل بدعة ضلالة وكل ضلالة في النار. أوصيكم ونفسي بتقوى الله عز وجل فإن للمتقين مفازا.***Ndugu zangu waislamu, Allah amesema katika Quran:﴿إِنَّ هَٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ ﴾. Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.Mitume na manabii wa tangu enzi za kale, pamoja na mataifa yao, hadi mtume wa mwisho Muhammad ﷺ na umma wake, ni sehemu ya umma mmoja. Hii ni kwa sababu mitume wote walikuja na ujumbe mmoja, nao ni wito wa Tawhid — kumtakasia Allah ibada pekee bila mshirika. Ulinganizi wao wa Tawhid umekuwa msingi wa kuundwa kwa waislamu wa vizazi vyote, tangu zama za kale hadi sasa.Waislamu wote, licha ya tofauti za wakati, maeneo, na tamaduni, wanashikamana na misingi inayofanana ya itikadi, matendo, na hata muonekano. Ingawa baadhi ya watu wamepotea njia kutokana na sababu mbalimbali, sura ya umoja na mshikamano wa waislamu inaendelea kudhihirika. Umoja huu unaitwa Undugu wa Kiislamu.﴿إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ﴾.Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Allah ili mrehemewe. 049:10Nasafi ya MtumeNdugu zangu Waislamu, tambueni kuwa sisi sote ni wafuasi wa Mtume wetu mpendwa, Muhammad ﷺ. Kwa hivyo, tunapopewa maelekezo kuhusu undugu wa Kiislamu, ni muhimu kufahamu kwamba Mtume ﷺ ndiye ndugu yetu wa kwanza katika imani. Yeye ndiye anayestahiki zaidi heshima na nafasi ya kwanza katika kuimarisha undugu huu wa Kiislamu. Tuzingatie mafundisho yake na tuishi kwa mshikamano, upendo, na uadilifu kama alivyotufundisha.Allah amesema:﴿النَّبِيُّ أَوْلَىٰ بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنفُسِهِمْ ۖ وَأَزْوَاجُهُ أُمَّهَاتُهُمْ ۗ﴾.Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao. 033:06Mtume ﷺ amesema:وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَالِدِهِ وَوَلَدِهِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ".صحيح الجامع“Naapa kwa ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, Hatoamini mmoja wenu mpaka niwe mpendwa kwake zaidi ya mzazi wake mwanawe na watu wote (wengine).” Swahih Aljami’Mtume ﷺ ameshafariki dunia, lakini mafundisho yake bado yapo nasi kama mwongozo wa maisha. Kila Muislamu anapaswa kuwa na shauku ya dhati katika kumkubali, kumtii, kumpenda, kumsadikisha, na kufuata yale aliyokuja nayo. Hii ni sehemu ya imani yetu kama ilivyoelekezwa wazi katika Qur'an Tukufu.﴿وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۖ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴾.Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Allah. Hakika Allah ni Mkali wa kuadhibu. 059:07Allah amesema:﴿مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّهَ ۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا﴾.Mwenye kumtii Mtume basi ndio amemtii Allah. Na anaye kengeuka, basi Sisi hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi wao. 004:80Ndugu zangu Waislamu, ushahidi mwingi kutoka katika Qur'an na Sunna, ikiwemo dalili ambazo hazikutajwa hapa, unaonyesha wazi nafasi ya kipekee aliyonayo Mtume ﷺ katika maisha yetu kama Waislamu. Ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunatanguliza haki ya Mtume ﷺ juu ya haki za watu wa karibu nasi, kwa kutambua hadhi yake ya juu na heshima anayostahili.Nafasi ya WaislamuMtume ﷺ amesema:المُسْلِمُ أخُو المُسْلِمِ لا يَظْلِمُهُ ولا يُسْلِمُهُ، ومَن كانَ في حاجَةِ أخِيهِ كانَ اللَّهُ في حاجَتِهِ، ومَن فَرَّجَ عن مُسْلِمٍ كُرْبَةً، فَرَّجَ اللَّهُ عنْه كُرْبَةً مِن كُرُباتِ يَومِ القِيامَةِ، ومَن سَتَرَ مُسْلِمًا سَتَرَهُ اللَّهُ يَومَ القِيامَةِ. رواه البخاري“Muislamu ni ndugu wa muislamu, hamdhulumu wala kumuacha katika dhulma. Na atayekuwa katika kutatua haja ya ndugu yake muislamu, Allah atakuwa katika kumtatulia haja yake. Na atayemfariji muislamu kwa tatizo lililompata. Allah atamfariji kwa kumuondolea matatizo ya siku ya kiyama. Na atayemsitiri muislamu Allah humsitiri siku ya kiyama.” Amepokea Al BukhariMuislamu anapaswa kuwa bega kwa bega na ndugu yake Muislamu anapokumbwa na shida. Si jambo zuri kufurahia matatizo ya Muislamu mwenzako, kwani ni mtihani kutoka kwa Allah. Aidha, hujui kama wewe pia unaweza kukumbwa na mtihani kama huo au hata mkubwa zaidi. Badala yake, saidiana naye kwa dua, ushauri, na msaada wa hali na mali ili kupata radhi za Allah. Mtume ﷺ amesema:مَثَلُ المُؤْمِنِينَ في تَوادِّهِمْ، وتَراحُمِهِمْ، وتَعاطُفِهِمْ مَثَلُ الجَسَدِ إذا اشْتَكى منه عُضْوٌ تَداعى له سائِرُ الجَسَدِ بالسَّهَرِ والْحُمّى. متفق عليه“Mfano wa kupendana na kuhurumiana kwa waumini, ni mfano wa mwili. Ukiwa na maumivu katika kiungo kimoja, mwili wote hukesha kwa maumivu na homa kwaajili ya kiungo kimoja.” Al Bukhari na MuslimUndugu wa imani ndio msingi wenye nguvu zaidi wa kuunganisha watu, kwa sababu ndio muhimili wa mafungamano yao. Ikiwa undugu huu utavunjika, basi uhusiano kati yao pia huvunjika, kwani kilichowaunganisha kimeondoka – nacho ni imani ya pamoja. Mfano wa hili ni kwamba Muislamu hatomrithi mzazi wake au mtoto wake ikiwa mmoja wao si Muislamu. Hii ni kwa sababu undugu wa kiimani, ambao ni wa kiwango cha juu zaidi, tayari umevunjika. Hakika, Allah ndiye Mwenye elimu kamilifu na sahihi zaidi.***الحمد لله رب العالمين والصلاة والسلام على رسول الله وعلى آله وصحبه ومن تبعهم بإحسان إلى يوم الدين وسلم تسليما كثيرا. أما بعد:Nafasi ya WazaziUislamu umehimiza sana kuwafanyia wema wazazi wawili, jambo ambalo limethibitishwa kwa dalili mbalimbali katika Quran na Sunna. Hii ni kwa sababu wazazi ndio ndugu wa karibu zaidi na mtu katika muktadha wa aina ya pili ya undugu mdogo. Allah ameeleza wazi katika Quran:Allah amesema:﴿وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَىٰ وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ﴾.Na tumemuusia mwanaadamu kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia): Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni kwangu Mimi ndiyo marudio. 031:14﴿وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ إِحْسَانًا ۖ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ كُرْهًا وَوَضَعَتْهُ كُرْهًا ۖ وَحَمْلُهُ وَفِصَالُهُ ثَلَاثُونَ شَهْرًا ۚ حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَبَلَغَ أَرْبَعِينَ سَنَةً قَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَصْلِحْ لِي فِي ذُرِّيَّتِي ۖ إِنِّي تُبْتُ إِلَيْكَ وَإِنِّي مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴾. Na tumemuusia mwanaadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa tabu, na akamzaa kwa tabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini. Hata anapo fika utu uzima wake, na akafikia miaka arobaini, husema: Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayo yapenda. Na unitengenezee watoto wangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu. 046:15Kuwaasi wazazi:Mtume ﷺ amesema:رضا اللهِ في رضا الوالدينِ وسخطُ اللهِ في سخطِ الوالدينِ. ابن حبان والبيهقي“Radhi za Allah (zimefungamana) na radhi za wazazi wawili na ghadhabu za Allah (zimefungamana) na ghadhabu za wazazi wawili.” Ibn Hibban na BayhaqiMtume ﷺ amesema tena:لا يدخُلُ الجنَّةَ عاقٌّ ولا منّانٌ ولا مُدمِنُ خمرٍ.ابن حبان“Haingii peponi muasi wa wazazi wazazi wawili, mbeya na mdumu kunywa pombe.” Ibn HibbanNdugu wengine wa karibu:Muislamu anapaswa kuheshimu haki za wazazi wawili, lakini pia asisahau wajibu wa kudumisha uhusiano wa undugu na watu wa karibu kama wanaukoo, jamaa wa ukweni, au wundugu kwa kunyonya pamoja. Ndugu baina yao wanapaswa:Kutembeleana na kujuliana hali, kuonyeshana upendo na kujali.Kusaidiana na kushirikiana katika shida na raha, kuwa bega kwa bega kila wakati.Kunasihiana, kusuluhishana, na kuombana msamaha pale kunapojitokeza migogoro.Kuheshimiana, kuhurumiana na kuthamini tofauti zao.Kufundisha watoto wetu umuhimu wa kutambuana, kuheshimiana na kuwa na mshikamano katika familia.Mtume ﷺ amesema:مَن أحَبَّ أنْ يُبْسَطَ له في رِزْقِهِ، ويُنْسَأَ له في أثَرِهِ، فَلْيَصِلْ رَحِمَهُ. متفق عليه“Apendaye kukunjuliwa riziki yake na kupewa nguvu katika athari yake (umri) basi aunge undugu.” Al Bukhari na MuslimUbaya wa kukata undugu.Kukata undugu si jambo baya tu, bali pia ni uasi kwa Allah na Mtume wake ﷺ. Hili ni jambo linalozingatiwa kuwa miongoni mwa madhambi makubwa. Allah Mtukufu amesema:﴿فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِنْ تَوَلَّيْتُمْ أَنْ تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ﴾.Basi mnatarajia mtawalapo ndio mfisidi katika nchi na muwatupe jamaa zenu? 047:22﴿أُولَئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَى أَبْصَارَهُمْ﴾. Hao ndio aliowalaani Allah, na akawatia uziwi, na akawapofoa macho yao. 047:23Na Mtume ﷺ amesema:لا يَدْخُلُ الجَنَّةَ قاطِعُ رَحِمٍ. مسلم“Haingii peponi mkata undugu.” Muslim.Kwa kuzingatia mafundisho ya Quran na Sunnah, kama ilivyoelezwa na wema waliotangulia, tunajifunza kuwa kuhifadhi na kulinda undugu ni jambo muhimu na limehimizwa sana. Kukata undugu ni mojawapo ya madhambi makubwa ambayo tumeonywa kuhusu. Tunapaswa kuwahimiza watu waendelee kushirikiana na kudumisha undugu wao, kwa kusalimiana na kuzungumza kama kawaida. Kwani Mtume ﷺ amesema:لا تَدْخُلُونَ الجَنَّةَ حتَّى تُؤْمِنُوا، ولا تُؤْمِنُوا حتَّى تَحابُّوا، أوَلا أدُلُّكُمْ علَى شيءٍ إذا فَعَلْتُمُوهُ تَحابَبْتُمْ؟ أفْشُوا السَّلامَ بيْنَكُمْ.Hamtoingia peponi mpaka muamini, Hamtoamini mpaka mpendane. Je nisiwafahamishe jambo ambalo mkilifanya mtapendana? Toleaneni salamu. 
Soma Makala
Fiqh Oct 22, 2026

Swala ya Maiti

Namna ya kumswalia MaitiUtasimama nyuma ya kichwa cha maiti mwanaume au katikati ya mwili wa maiti mwanamke.Utasema “Allahu Akbar” [Takbira ya kwanza] huku ukinyanyua mikono usawa wa mabega na kufunga swala kwa kuweka mkono wa kulia juu ya wa mkono wa kushoto kifuani wako . Utasoma Surat Al Fatihah na Sura nyingine utayoichagua kwa siri. Kisha utasema “Allahu Akbar” [Takbira ya pili] (Lakini hautanyanyua tena mikono kama kwenye Takbir ya kwanza). Kisha utamswalia Mtume Muhammad kwa kusema:(اللهم صل على محمد وعلى آل محمد كما صليت على إبراهيم وعلى آل إبراهيم إنك حميد مجيد، اللهم بارك على محمد وعلى آل محمد كما باركت على إبراهيم وعلى آل إبراهيم إنك حميد مجيد)Kisha utasema “Allahu Akbar” [Takbira ya tatu] kama takbir ya pili, Kisha utasema dua hii:اللهم اغفر له وارحمه ، وعافه واعف عنه ، وأكرم نزله ، ووسع مدخله ، واغسله بماء وثلج وبرد ، ونقه من الخطايا كما ينقى الثوب الأبيض من الدنس ، وأبدله دارا خيرا من داره ، وأهلا خيرا من أهله ، وزوجا خيرا من زوجه ، وأدخله الجنة وأعذه من عذاب القبر ،ومن عذاب النار .***اللهم اغفر لحينا وميتنا ، وشاهدنا وغائبنا ، وصغيرنا وكبيرنا ، وذكرنا وأنثانا ، اللهم من أحييته منا فأحيه على الإسلام ، ومن توفيته منا فتوفه على الإيمان. ***اللهم لا تحرمنا أجره ، ولا تضلنا بعده. ***اللهم إن فلان ابن فلان في ذمتك وحبل جوارك، فقه من فتنة القبر، وعذاب النار، وأنت أهل الوفاء والحق، فأغفر له وارحمه، إنك أنت الغفور الرحيم.Ikiwa maiti ni Mtoto sema baada ya dua hizo:اللهم اجعله سلفاً لوالديه ، وفرطاً وأجرا.***Kisha utasema “Allahu Akbar” [Takbira ya nne] atasubiri kidogo kisha utatoa salamu moja kuliani kwako (Akitoa salamu mbili hakuna ubaya).
Soma Makala

Darsa za Sauti (Audio Series)

Sikiliza Zote
Quran

Usul Thalatha

Tawheed

Kitabu Tawhid

Quran

Mansour Al-Salimi

Muda wa Swala (Prayer Times - Tanzania)

Dar es Salaam, Tanzania
Inapakia muda wa swala...
Masjid Al-Haram Makkah
Masjid Al-Haram - Makkah

Toa Maoni Yako ya Kheri (Share Your Comments)

Maoni ya Hivi Punde (Recent Comments)

U
Ummu Issa
Oct 23, 2026

"Assalamu alaykum. Na sisi tunaotaka kusoma dini, mtutengeneze mfumo wa kusoma online... wengine sie tumeajiriwa. baraka llahu fiikum"

Imeidhinishwa
A
Abu Hassan Farhan
Oct 23, 2026

"MashaAllah, Hii ni platform ya kisasa sana, Mungu Awabariki."

Imeidhinishwa